Matofali ya kuchoma na Matumizi yake.
Ujenzi wa kisasa umebadilika sana, kutokana na mabadiliko mbali mbali ya kiteknolojia, watu wamelazimika kubadilika sawa sawa na mabadiliko haya ya Teknolojia.
Katika Ujenzi wa nyumba bora, kama mjenzi kuna mambo mbali mbali unapaswa kutia manani kabla na wakati wa ujenzi, mambo haya yakiwa kama, Joto la eneo la ujenzi, Ukubwa wa kiwanja, aina ya udongo wa kiwanja, Muinuko wa eneo wa Ujenzi, aina la jengo, na aina ya malighafi yatumikapo katika ujenzi, mambo haya bila kutiwa manani yanaweza kuathiri ujenzi wako. Na kwa hivyo katika Ujenzi wa jengo bora waatalamu wa matofali ya kuchoma wametafiti na kugundua aina tofauti ya matofali ya kuchoma na matumizi yao katika Ujenzi.
Matofali ya Kuchoma aina ya Roma (Roman).
Matofali ya kuchoma aina ya Roma,yaligundulika kwa mara ya kwanza katika jiji la Roma lililoko maeneo ya Italia Ulaya. Matofali haya huwa ni miembamba na ya kunyooka. mara nyingi matofali haya huwa kati ya size ya inchi 2inx12inx4in. Kutokana na muundo wake mwembamba na kunyooka matofali haya hutumika na wajenzi katika kufanya Upambaji au Urembo wa Mwisho wa nyumba au finishing, Matofali haya ni maarufu katika kuremba ukuta wa njee, jikoni, vyumbani na maeneo ya sebule.
Matofali ya kuchoma aina ya Norma ( Norman).
Matofali ya kuchoma ya norma ( Norman ) yaligundulika kwa mara ya kwanza katika kipindi cha 900- 1000 AD na kabila ya Norma iliyokuwa na makazi yake katika maeneo ya Ufaransa, Kabila hili ilisambaa na katika kusambaa kwao walisambaza pia ujuzi wa matofali yao ya kuchoma . Matofali haya ya Norma hayana utofauti sana na matofali ya Roma isipokuwa urefu na size yake ikiwa 2 2/3in x12in x 4 in ukilinganisha na Saizi ya Matofali ya Roma ilikuwa na saizi ya 2 in x 12 in x 4 in. Pamoja na hayo matofali haya huwa na matobo ya miraba minne (rectangular) katika maeneo ya juu ya matofali haya ikiwa pia ndo tofauti kubwa kati yake na Matofali ya kuchoma ya Roma.
Matofali ya kuchoma aina ya Meridian ( Meridian).
Matofali haya ni matofali yenye utofauti kidogo na matofali aina ya Utility na Norma. Matofali haya na marefu na membamba yenye saizi ya inchi 4 in x 16 in x 4 in. Matofali haya yana matobo mengi ya mviringo katika maeneo yake ya juu. Matobo haya hutumika katika ujenzi kuongeza mshikamano kati ya tofali na Seruji. matofali haya hujazwa seruji katika matundu yake kuongeza uimara na mshikamano kati ya tofali moja na ingine ikiwemo na seruji pia, Matofali haya hutumika zaidi katika ujenzi wa majengo makubwa yenye uhitaji wa kuwekewa uimara ili kuweza kukabiliana na uzito mkubwa wa jengo hivyo matundu haya katika matofali haya hutumika kuongezea uimara katika msingi pamoja na muinuko wa jengo.
Matofali ya kuchoma aina ya Utility.(Utility)
Matofali haya ya Utility ni matofali madogo kidogo ukilingisha na Matofali ya Kuchoma aina ya Meridian, Utofauti huu hutokana saizi yake ikiwa matofali haya ni mafupi na yako katika saizi ya inchi 4 in x12 in x 4 in, ukilinganisha na matofali ya kuchoma aina ya meridian ambayo ni saizi inchi 4 in x16 in x 4 in.Matofali haya kutokana na ufupi wake huwa na matundu machache kwa juu ukilinganisha na matofali ya meridian. Matofali haya huutumika zaidi katika ujenzi wa eneo ya milango na maeneo ya madirisha ya Jengo.
Matofali ya kuchoma aina ya Double through wall Meridian.
Matofali haya ni miongoni ya matofali yenye ukubwa sana. Matofali haya ukilinganisha na aina zingine zina urefu pamoja na uwima mkubwa kuliko matofali ya aina zingine kwa inchi 8 inx 16 inx 4 in matofali haya yana matundu makubwa ambayo zege nene hupitishwa katika matundu yake matofali haya pia hutumika kwenye ujenzi katika maeneno yenye udongo wa kutitia. zege humwagwa kwenye matofali haya kutengenza uimara katika jengo.
Matofali ya kuchoma yako ya aina nyingi, na ni muhimu kuwa na ufahamu kabla ya kujenga jengo lako. Hivyo kwa Ushauri wa matofali ya kuchoma , pamoja na matofali ya kuchoma bora na imara wasiliana nasi kupitia 06555 3560 33/ 0754 316 033 Arusha, Tanzania.