Faida ya Kujenga kwa Matofali ya Kuchoma.
Kuwa na nyumba ni malengo ya watanzania wengi.Iwe ni kwa kuanza maisha, kuanza familia na muenzi wako, au kuweza kuhama katika nyumba ya kupanga na kuwa na mahali utakapoita nyumbani. Nyumba ina umuhimu sana katika maisha ya wanadamu, na kwa wengi ni malengo yao kuu. Kujenga Nyumba bora iliyoimara inahitaji umakini sana katika kujenga na kupanga ujenzi wa nyumba yako ijayo. Hivyo ni muhimu sana kujua aina ya matofali bora katika ujenzi wa Nyumba ya ndoto zako. Hivyo leo nitakueleza faida za kujenga kwa matofali ya kuchoma.
Matofali ya kuchoma haina gharama.
Ujenzi wa matofali wa kuchoma ni ujenzi ya bei nafuu na hauhitaji kipato kikubwa kujenga nyumba kwa matofali ya kuchoma, gharama hio huwa ndogo kutokana na gharama ndogo ya matofali hayo ambayo huwa kati ya 400 hadi 600 katika bei ya soko ukilinganisha na gharama ya tofali ya cement ambayo gharama yake huenda hadi sh. 2200 kwa tofali moja katika bei la soko.Matofali hayo hayahitaji watu wengi kwenye kujenga kwa kuwa hazina uzito mkubwa, ujenzi wake hauitaji watu wengi hivyo gharama ya kujenga hupungua.
Matofali ya kuchoma ni Imara.
Matofali ya kuchoma yanauwezo wa kudumu kwa miaka mingi kuliko matofali ya cement. Kwa kawaida matofali ya kuchoma yanauweza kwa kudumu kwa miaka hadi mia tatu bila kuharibika wala bubujuka. Ulikilinganisha na matofali ya cement ambayo kudumu kwake ni kati ya miaka sitini hadi mia.Hivyo nyumba ya matofali ya kuchoma inauwezo wa kudumu kwa miaka mingi zaidi kuliko ya cementi.
Matofali ya kuchoma yana muonekano mzuri.
Matofali ya kuchoma huwa na muonekano mzuri wa kuvutia,Matofali ya kuchoma hayahitaji rangi wala finishing kufanya eneo la nyumba kupendeza, bali matofali haya yanauwezo mkubwa wakutunza mvuto wake kama rangi na muundo, kwa miaka mingi bila kupoteza uhalisia na upya wake. Ndio maana eneo lijengwalo kwa matofali ya kuchoma linauwezo wakuonekana kwamba ni mpya ingawa inamiaka mingi.
Hivyo ni vyema kuchanganua na kufahamu ubora na umuhimu wa matofali ya kuchoma katika ujenzi wa nyumba bora na imara. Kwa kuwa wengi wanandoto za kuwa na nyumba iliyo na mvuto,hivyo matofali ya kuchoma ndio suhuluhisho hilo.
Kwa ushauri kuhusu Matofali ya Kuchoma. Pamoja na matofali imara. Wasiliana nasi kupitia: +255 655 356 033, +255 754 316033.
Asanteni Sana!!!